Kumekucha blog
Watch here
Wednesday, March 8, 2017
Rostov kuwakabili Manchester United - Europa Ligi
Ikumbukwe kuwa mnamo mwezi wa 11 mwaka 2016 wenyeji hawa wa Rostov waliinyuka Bayern Munich ya ujerumani goli 3:2
Monday, June 20, 2016
Serikali yasitisha ajira zote
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam SERIKALI imesitisha ajira zote, kama njia ya kukabiliana na wimbi la watumishi hewa. Kutokana na uamuzi huo hivi sasa hakuna nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa Serikali na wakala zake pamoja na utoaji wa vibali wa likizo ya bila malipo. Akizungumza na MTANZANIA jana jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu Utumishi, Dk. Laurean Ndumbaro, alisema kuwa Serikali imesitisha kwa muda utoaji wa ajira, ili kupitia upya muundo wa Serikali na taasisi zake. Alisema utekelezaji wa mkakati huo utakwenda sambamba na kusitisha kwa muda utoaji wa vibali vya ajira zote mbadala pamoja na uidhinishaji wa ajira hizo zilizopo Sekreterieti ya Ajira katika utumishi wa umma na kwenye mfumo wa taarifa za kiutumishi. “Ni kweli tumesitisha kwa muda ili kupitia mfumo wa Serikali na hata kuangalia ulipaji wa mishahara kama upo katika malipo stahiki. “…na hili litakwenda sambamba na hata kusitishwa malipo ya mishahara yanayotokana na upandishwaji wa vyeo kwa watumishi. Tukimaliza zoezi hili ndipo tunaweza kuanza kutoa ajira za Serikali,” alisema Dk. Ndumbaro. Alisema muundo mpya wa utumishi wa Serikali unakwenda sambamba na uhakiki wa malipo ya mishahara, hivyo ni lazima ujue ni nani unayemlipa kuliko ilivyo sasa. Kwa mujibu wa maelekezo hayo uhamisho na uidhinishaji katika mfumo wa watumishi ambao wamehamishwa kutoka kwa mwajiri mmoja kwenda kwa mwajiri mwingine ambao atalipwa mshahara mkubwa kuliko ule wa sasa pia utaangaliwa kwa lengo la kupata taarifa sahihi za mtumishi husika. “Baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki watumishi pamoja na tathmini ya muundo wa Serikali na taasisi zake, wote wataarifiwa ni lini utekelezaji utaendelea,” alisema. Taarifa kutoka maeneo mbalimbali nchini, zililiambia gazeti hili kuwa maelekezo hayo yalitolewa Juni 13, mwaka huu na kusambazwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo kwa makatibu wakuu wote, makatibu tawala wa mikoa, kwa wakuu wa idara za Serikali zinazojitegemea. Waliotakiwa kutekeleza maelekeo hayo ya Serikali ni wakurugenzi wote wa majiji, manispaa na miji, wakurugenzi watendaji wa halmashauri za wilaya, watendaji wa taasisi za umma na watendaji wa wakala za Serikali kwa upande wa Tanzania Bara.
Sunday, June 19, 2016
Rooney wants new deal.
Wayne Rooney prepared to end career at Manchester United.
Wayne Rooney said he was happy to extend his contract at Manchester United Wayne Rooney said he was happy to extend his contract at Manchester United Wayne Rooney would be happy to sign a new contract at Manchester United and end his playing career at Old Trafford. The 30-year-old has three seasons left on his current deal but believes he can go on for longer after former United manager Louis van Gaal moved him into a deeper central midfield role last season. Manchester United captain Wayne Rooney says he is looking forward to working with Jose Mourinho next season Manchester United captain Wayne Rooney says he is looking forward to working with Jose Mourinho next season According to the Sun on Sunday, Rooney has now said he would be willing to extend his current deal and see out his playing days at the club.
Algeria yafunga mitandao kuzuia udanganyifu kwenye mitihani
Algeria imefunga kwa muda mitandao ya kijamii kote nchini katika jitihada za kuzuia wizi wa mitihani ya shule za upili. Karibu nusu ya wanafunzi walilazimishwa kurudia mtihani huo kuanzia leo Jumapili, baada ya mtihani wa kwanza kukumbwa na udanganyifu kwa njia ya mitandao. Wanafunzi wengi walifanikiwa kupata maswali kwa njia ya mtandao wa Facebook na mitandao mingine kabla ya kufanyika kwa mtihani huo. Hatua ya kufunga mitandao ya kijamii ililenga kuwalinda wanafunzi kutokana na kuchapisha maswali yasiyo sahihi kupitia kwa mitandao hiyo.
WATOTO WA RAIS KAGAME WAICHEZEA TIMU YA RWANDA
Kwa mara ya Kwanza wanawe rais wa Rwanda Paul Kagame, Bryan Kagame na Ian Kagame waliiwakilisha timu ya taifa ya Rwanda kwa wachezaji wasiozidi miaka 20 katika mechi ya kuadhimisha miaka 22 tangu mauaji ya kimbari nchini Rwanda. Mchuano huo wa kumbukumbu, kati ya Rwanda na Morocco ulioandaliwa katika uwanja wa Amahoro, mjini Kigali ulikamilika kwa sare ya goli moja. Ingawa wote wawili hawakukamilisha mechi hiyo. Kocha wa Rwanda Kayiranga Jean Baptista aliwapa nafasi ikiwa ni mechi yao ya kwanza kuvaa sare ya timu ya taifa ya soka. Ian Kigenza Kagame alijumuishwa katika kikosi kilichoanza kabla ya kumpisha Park Udahemuka kunako dakika ya 27. Rwanda maarufu nyigu wachanga walitangulia katika dakika ya kwanza kupitia Blaise Itangishaka. Hata hivyo Morocco ilisawazisha katika dakika ya 43 baada ya Morocco Dari Achraf kumuandalia krosi Hicham Boussoufiane. Kunako dakika ya 74, Kitinda mimba wa familia ya kagame, Bryan Kagame alichukua nafasi yake Djabel Manishimwe. Baba yao wawili hao, Rais Paul Kagame ni shabiki wa soka na tenisi na ni shabiki sugu wa klabu ya Arsenal ya Uingereza.
Sunderland midfielder Emanuele Giaccherini would welcome Chelsea move, says agent
Mashabiki Wapagawa na Albam Mpya ya Beyonce
Albamu mpya ya Lemonade iliotolewa na Beyonce Knowles imeorodheshwa miongoni mwa albamu zilizopendwa sana baada ya kutolewa mwaka huu,lakini ,kipande cha albamu hiyo kilichotolewa wiki moja kabla ya uwepo wa albamu hiyo kufichwa hadi wakati wa toleo la filamu fupi lililoandamana na albamu hiyo kimezua utata. Kipande hicho cha albamu hiyo kilishirikisha msururu wa vipande vifupi vifupi vya albamu hiyo bila maelezo ,vingi vikimuonyesha Beyonce na kumalizika kwa maelezo yaliosema :Lemonade A world Permier event. Na sasa mtengezaji huru wa filamu kwa jina Matthew Fulks anadai kuwa kipande hicho kilinakili mojawapo ya kazi zake kwa jina Palinoia. Fulks anadai kwamba kampuni ya muziki ya Sony ile ya Columbia Recordings pamoja na ile ya Beyonce Parkwood Entertainment zilijua kuhusu kazi yake kabla ya utengezaji wa Lemonade ulipoanza na kwamba walishawishiwa na kazi yake. Anasema kuwa kipande hicho cha albamu ya Lemonade kinafanana na kile cha Palinoia ambayo ni kazi yake. Anaongezea kuwa baadhi ya vitu vinavyofanana kati ya filamu hizo mbili ni pamoja na michoro katika ukuta,watu wenye macho mekundu na picha zilizopigwa katika ngazi pamoja na eneo la kuegesha magri chini ya nyumba.